Jukwaa latangaza maazimio 7 kumuunga mkono Samia uchaguzi mkuu

DAR ES SALAAM: JUKWAA la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam limetangaza maazimio saba ya kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Wanawake hao pia wameeleza dhamira yao ya kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha Rais Samia anarejea madarakani kwa ushindi wa kishindo, wakisema amekuwa kinara wa maendeleo na mtetezi wa wanawake nchini.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Juni 15, Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Rehema Sanga amesema wanawake hao wameungana kwa sauti moja kutokana na imani yao kwa uongozi wa Rais Samia.

“Tunaona fahari kuwa na Rais mwanamke ambaye amefungua fursa za kiuchumi kwa wanawake, amesimamia amani, na ameleta mageuzi ya kweli katika sekta mbalimbali. hatuna sababu ya kutoyatangaza mafanikio haya na kuhakikisha anaendelea kuongoza taifa letu,” amesema Rehema.

Akizungumzia maazimio hayo, Rehema amesema yamelenga kuonyesha mshikamano kueneza mafanikio ya serikali, na kushiriki kikamilifu katika harakati za uchaguzi mkuu.

Amebainisha kuwa wanawake hao wataendelea kumuunga mkono Samia ambaye pia ni mlezi wa jukwaa hilo, na kusimama imara nyuma yake katika kuliongoza taifa.

“Tutaunga mkono juhudi zote za Rais Samia katika kujenga Tanzania yenye amani, utulivu, maendeleo endelevu na ustawi wa kijamii, kiuchumi na kisiasa,” amesisitiza.

Amesema azimio jingine ni kutangaza kwa nguvu zote mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia, kwa kutumia kila jukwaa linalowezekana kuanzia mitandaoni hadi mikusanyiko ya kijamii.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button