Samia: Mabadiliko ya Katiba 2025-2030

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa suala la mabadiliko ya Katiba lipo kwenye ajenda ya serikali na litatekelezwa ndani ya kipindi cha mwaka 2025 hadi 2030, sambamba na maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Akihutubia Bunge leo Juni 27, 2025, Rais Samia alieleza kuwa serikali inalipa uzito suala hilo na itaendelea kulishughulikia kwa umakini na maridhiano ya kitaifa ili kuhakikisha linaendeshwa kwa maslahi ya Watanzania wote.

“Suala la mabadiliko ya Katiba lipo, na litashughulikiwa katika kipindi cha 2025–2030, kwa kuwa pia ni sehemu ya Ilani ya CCM,” alisema Rais Samia.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button