Wasafiri zaidi ya milioni 2 wametumia SGR

 

DODOMA: RAIS Samia Suluhu Hassan amesema ujio wa safari za treni ya kisasa ya SGR umeleta tija kubwa kiuchumi.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo Juni 27 wakati akifunga Bunge la 12 la Tanzania, Rais Samia amesema tangu kuanza kwa safari za treni hizo mwezi Agosti mwaka 2024 manufaa mengi yameonekana.

Rais amesema zaidi ya  ya wasafiri milioni mbili wametumia usafiri huo huku ukusanyaji wa maduhuli ukifikia Sh bilioni 60.88.

Ameongeza kuwa wasafiri kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma wananufaika na matumizi ya muda mchache wa safari zao.

“Saa za safari za Dar es Salaam kwenda Dodoma( Dodoma- Dar) zimepungua kutoka saa nane hadi saa tatu tu, ninaambiwa hapa wabunge mnalala Dar es Salaam na mnaamka Dodoma hapa asubuhi” amesema Rais Samia.

Pia Rais amesema Serikali inaendelea na ukamilishaji wa vipande vingine ili Wananchi wa maeneo mengine waonje matunda yake.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button