NGOs waagizwa mikakati utekelezaji miradi

MTWARA: MASHIRIKA mbalimbali yasiyo ya Kiserikali (NGOs) mkoani Mtwara yametakiwa kuanza kutengeneza mkakati wa kutumia mapato ya ndani ili kuzalisha fedha na kufanya miradi endelevu zaidi badala ya kusubiri fedha kutoka kwa wafadhili.

Hayo yamejiri wakati wa jukwaa la mashirika hayo yasiyo ya kiserikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani humo lililofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani kuhusu kujadili kwa pamoja namna watakavyo boresha zaidi kazi zao hizo.

Akizungumza wakati wa jukwaa hilo, Mwakilishi wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na masuala mbalimbali ya kijamii mkoani Mtwara (FAWOPA) Baltazar Komba amesema lengo la kuweka jukwaa hilo ni kujadili kwa pamoja na wadau namna watakavyo boresha kazi zao zaidi ili kuwavutia wafadhili wengi katika sekta hiyo.

Jukwaa hilo limeandaliwa na Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) kwa kushirikiana na ofisi ya msajili wa mashirika hayo mkoani Mtwara na kukutanisha wadau, mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya kiserikali ili kufanya tathimini ya mashirika hayo katika kuchangia maendeleo ya taifa ya mwaka 2020/2021 na 2024/2025.

“Mashirika yaanze kutengeneza mkakati wa kutumia mapato ya ndani ili kuzalisha fedha na kufanya miradi endelevu zaidi”amesema Komba

Baadhi ya washiriki wa Jukwaa hilo akiwemo Shakila Mpomo kutoka shirika la FB Empowerment mkoani humo amesema mashirika yana mchango mkubwa katika kutoa huduma kwa jamii hasa zile zilizopo pembezoni.

“NGOs tuna fursa ya kufanya miradi ya kibiashara ili tuweze kujipatia fedha bila kusubiria fedha kutoka kwa wafadhiri wa mashirika”amesitisiza shakila

Mashiriki mwimgine Justin Kabelege, amesema katika tathimini iliyofanyika kwenye jukwaa hilo amejifunza kuhusu namna ya kushirikiana na taasisi mbalimbali ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili kuzuia rushwa kwenye mashirika jambo litaloimarisha utendaji bora wa kazi kwa wafanyakazi.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button