RC Arusha apokea ujumbe wa IPU

MKUU wa Mkoa wa Arusha, CPA Amos Makalla mapema leo Desemba 04, 2025 ameupokea na kuzungumza na Ujumbe wa Umoja wa Mabunge duniani (IPU), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano mkubwa wa mabunge unaotarajiwa kufanyika mkoani Arusha na kuhusisha maspika, wabunge na viongozi zaidi ya 1500 kutoka kote duniani.

Ujumbe wa IPU umeongozwa na Balozi Ande Filip, akiwa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa Geneva, Uswisi Dk Hoyce Temu ambapo katika maelezo yake Balozi Ande amesema katika mkutano huo, mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan.

SOMA: RC Makalla : Utalii Arusha wazidi kuimarika

“Tanzania ni Mwenyeji na sababu kubwa ni ushiriki na historia yake katika IPU na kikubwa zaidi ni namna wao wanavyoiona Tanzania na sisi tumewahakikishia tupo tayari kuwapa ushirikiano kufanikisha mkutano huo mkubwa wa Kihistoria,” amesema Makalla.

Makalla amesema mkutano huo ni fursa kwa wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla na ukija wakati mzuri katika kudhihirisha amani, usalama na utulivu uliopo nchini na kuaminika kwa Tanzania kimataifa, akiwataka wananchi kujiandaa kutumia fursa za ujio wa mkutano huo kiuchumi.

Kwa Upande wake Balozi Ande kwa niaba ya maafisa wengine wa IPU, amesema mkutano huo wa kimataifa utafanyika kwa siku sita jijini Arusha na kulingana na ratiba.

Amesema washiriki wake kutoka kote duniani watakuwa na zaidi ya siku sita mkoani humo ili kuwapa fursa ya kutembelea maeneo ya kihistoria na vivutio vya Utalii vilivyopo Arusha na maeneo mengine ya jirani.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. I am making a good salary from home $7580-$9065/week , which is amazing, under a year ago I was jobless in a horrible economy. I thank God every day I was blessed with these instructions, Definitely a try..

    See This Link………………………………….. http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button