Macron, Putin wazungumza baada ya miaka miwili

PARIS : RAIS wa Ufaransa Emmanuel Macron na mwenzake wa Urusi, Vladimir Putin, wamezungumza kwa simu kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka miwili na nusu, wakijadili hali ya Ukraine na masuala ya kimataifa.

Katika mazungumzo hayo ya zaidi ya saa mbili, Macron alimhimiza Putin kusitisha vita nchini Ukraine, akisisitiza haja ya kupatikana kwa suluhisho la amani. Hata hivyo, Putin alishutumu mataifa ya Magharibi kwa kuchochea mzozo huo.

Kwa mujibu wa Ikulu ya Elysee, viongozi hao walikubaliana kuendeleza mawasiliano kuhusu Ukraine na Iran, ikiwa ni hatua ya kutafuta mwafaka wa kidiplomasia.

Taarifa kutoka Ikulu ya Kremlin imesema Putin alieleza kuwa mzozo wa Ukraine umetokana na sera za mataifa ya Magharibi, na kwamba makubaliano yoyote ya amani yanapaswa kuwa ya kina, ya muda mrefu na kushughulikia mizizi ya mgogoro huo.

Mazungumzo haya yanachukuliwa kuwa ni mwanzo mpya wa mawasiliano kati ya viongozi hao wawili, baada ya miaka ya mvutano uliochochewa na vita inayoendelea mashariki mwa Ulaya. SOMA: Marekani, Ulaya, Ukraine kujadili mzozo wa Urusi


 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button