Watu 248 wauawa Syria

DAMASCUS : TAKRIBAN watu 248 wameuawa katika mfululizo wa mapigano yaliyodumu kwa siku kadhaa huko Sweida, Kusini mwa Syria, hali iliyoilazimu serikali kutuma vikosi vya usalama kudhibiti machafuko hayo.
Kwa mujibu wa Shirika la Syria Observatory for Human Rights, waliouawa ni pamoja na wanachama 92 wa jamii ya wachache ya Druze, wakiwemo raia 28. Taarifa zinaeleza kuwa watu 21 waliuawa kwa maagizo ya moja kwa moja ya vikosi vya serikali.
Katika mapigano hayo pia, maafisa 138 wa usalama wa serikali ya Syria waliripotiwa kuuawa, sambamba na wapiganaji 18 wa kutoka jamii ya Bedouin. Taarifa hizo zimeibua hofu ya kuzuka kwa mzozo mkubwa wa kijamii na kiusalama katika eneo hilo lenye historia ya kutulia.



