Ethiopia yakamata watu 82 wa IS

ADDIS, ETHIOPIA : MAMLAKA za Ethiopia zimewakamata watu 82 wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu (IS), ambao inadaiwa walipokea mafunzo katika jimbo la Puntland nchini Somalia kwa lengo la kufanya mashambulizi ndani ya Ethiopia.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fana kupitia huduma ya ujasusi ya kitaifa (NISS) imekuwa ikifuatilia kwa muda mrefu mikakati ya kundi hilo ya kupenyeza ndani ya mipaka ya nchi na kuanzisha vikundi vya wanamgambo wanaopokea maagizo kutoka IS.

Taarifa zinaeleza kuwa kundi hilo linahusiana moja kwa moja na IS nchini Somalia, ambalo linaaminika kuwa na kati ya wapiganaji 700 hadi 1,500. Kwa miaka ya hivi karibuni. Kwa sasa tawi hilo limeendelea kuimarika kutokana na ongezeko la wapiganaji wa kigeni pamoja na vyanzo vya mapato ya kudumu.

SOMA: Somalia Ethiopia kumaliza mivutano

Haya yanajiri siku moja tu baada ya mashambulizi ya Marekani kuwaua baadhi ya viongozi wa IS nchini Somalia, akiwemo mphttps://habarileo.co.tz/somalia-ethiopia-kumaliza-mivutano-ya-kikanda/anga mikakati wa kundi hilo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kimataifa kupunguza ushawishi wa IS katika ukanda wa Afrika.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button