Takukuru Shinyanga kujizatiti udhibiti rushwa

SHINYANGA: TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Shinyanga imeeleza serikali kuendelea kuimarisha mifumo mizuri na kuziba mianya ya utoaji rushwa kwa kuhakikisha unakuwepo uimara thabiti.
Hayo yamesemwa na Ofisa Takukuru mkoani hapa, Mohamed Doo kwenye kikao wakati akiwasilisha mada juu ya kuzuia na kupambana na vitendo vya rushwa kwa wamiliki wa vituo vya kulea watoto mchana na makao ya watoto wanao ishi kwenye mazingira magumu.
Doo akizungumza na wamiliki hao amesema Programu Jumuishi ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) ni zuri imeleta wadau pamoja lakini suala la kukemea vitendo vya rushwa watoto wadogo waanze kufundishwa kupitia nyimbo nzuri zenye maudhui ya kupinga.

Doo amesema watu wamejenga desturi ya kuhalalisha rushwa ili apate kitu kizuri na urahisi nakujaribu kutumia njia ya mkato na ushawishi ili wapate kile walichokusudia hayo yote kwenye jamii kukubali pasipo kutoa taarifa kwenye mamlaka.
“Tumekuwa tukishtaki watuhumiwa wanaoendesha vitendo vya rushwa kwa watumishi wa taasisi za serikali na taasisi binafsi kwani watu wanajihusisha wanapobainika wanachukuliwa hatua,” amesema Doo.
Ameongeza “sisi tunapokea taarifa nyingi kutoka maeneo tofauti tofauti kwani zipo baadhi ya familia zinazotoa hongo ili watoto wao waliopo kwenye vituo walelewe vizuri zaidi kuliko wengine kwa kufanya hivyo hutamjenga itaonyesha kubaguliwa au kujibagua kwa mtoto mwenyewe nakujiona mnyonge.
Doo amesema zipo rushwa zinazotolewa kwenye vituo kama misaada hasa kwa watoto wanao lelewa kwenye makao na vituo kwa malengo yao mahususi na mbinu hizo zimekuwa zikitumika na matokeo yake kuleta maadili yasiyo faa kwa watoto.
Doo amesema wahudumu wanapopatika kwa njia ya ajira isiyo sahihi na wakati huo hawana sifa matokeo yake watoto kulelewa kinyume na maadili yaliyokusudiwa katika jamii na taifa kwa ujumla.



