KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025: Kataa siasa za uchochezi, hoja za chuki

WATANZANIA wanaelekea katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Oktoba 2025 hivyo, hawana budi kufungua macho na akili zao zaidi ili fursa ya uchaguzi isiwe laana kama inavyotokea kwa baadhi ya nchi duniani zikiwamo za Afrika, bali iwe neema.

Hii ni kwa kuwa katika kipindi cha uchaguzi, taifa hukutana na fursa kubwa ya kuimarisha demokrasia, lakini pia hukabiliwa na hatari ya migawanyiko iwapo siasa zitatumika vibaya hivyo, akili za wananchi hazina budi wakati wote kuwa macho ili uchaguzi utumike kuwajenga badala ya kuwabomoa.

Ikumbukwe kuwa, katika kipindi kama hiki, siasa za chuki na uchochezi huwa na nafasi ya kuibuka kwa kasi hasa zinapokuta akili za wananchi ‘zimelala usingizi’ au ‘zimezimia’ hivyo, kusababisha uhasama, vurugu na kuvunjika kwa amani na mshikamano wa kitaifa.

Kwa msingi huo, ni muhimu kuelewa kwamba uchaguzi ni chombo cha maendeleo, si silaha ya uharibifu na maangamizi ya watu wakiwamo ndugu wadamu eti kwa sababu ya tofauti za kimtazamo maana taifa halijengwi kwa kura tu, bali na hali ya umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi wote, hata wakiwa na mitazamo tofauti ya kisiasa.

Athari za siasa za uchochezi na hoja za chuki wa maendeleo ya taifa Siasa za uchochezi na hoja za chuki zinaathiri sana uwezo wa wananchi kubeba mzigo wa taifa na misingi ya maendeleo ya nchi. Hii ni kwa sababu zinavuruga umoja, kuaminiana na ushirikiano ambavyo ni nguzo muhimu katika ujenzi wa taifa.

Kimsingi, zipo namna nyingi ambavyo siasa za uchochezi na hoja za chuki zinavyoathiri maendeleo ya taifa

Kuvuruga umojawa kitaifa
Uchochezi hujenga migawanyiko ya kikabila, dini, kikanda na itikadi. Husababisha wananchi kuacha kujiona wamoja na badala yake, hujikita kwenye makundi yanayopingana kwa maslahi binafsi. Bila mshikamano hakuna ushirikiano wa kubeba mzigo wa taifa.

Hivyo, siasa za uchochezi na hoja za chuki ni sumu kwa maendeleo ya taifa kwa kuwa huathiri na kuvuruga umoja wa kitaifa.

Kudhofisha uaminifukwa taasisi za umma
Maneno ya chuki dhidi ya serikali au taasisi za umma hueneza kutoaminiana baina ya wananchi na serikali, hivyo huchochea watu kutokuwa na imani na taasisi za umma na kuzorotesha ushirikiano baina ya wananchi na taasisi za umma na kusababisha kutofikia malengo ya maendeleo kwa wakati.

Siasa za uchochezi na hoja za chuki husababisha wananchi kuacha majukumu na wajibu wao kama kulipa kodi, kutii sheria au kushiriki katika michakato ya kitaifa. Husababisha taifa kuingia katika mzunguko wa hasara, lawama na migogoro. Siasa za uchochezi na hoja za chuki ni chanzo cha migogoro na udidimizaji wa maendeleo ya nchi.

Kuzuia ushiriki wa wananchi katika maendeleo
Siasa za ‘majitaka’ zinazohusisha uchochezi huwatisha au kuwagawa wananchi na kuwafanya washindwe kushirikiana katika miradi ya kijamii, maendeleo au mipango ya serikali. Hoja za chuki huathiri vibaya ari ya vijana, wanawake na makundi mengine ya wananchi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa nchi yao.

Hali hiyo husababisha kusuasua kwa maendeleo ya nchi na wananchi wenyewe

Kupoteza amani na utulivu
Amani ni msingi wa maendeleo. Uchochezi huleta maandamano ya vurugu, hujenga uhasama wa kisiasa au makundi katika jamii na pia huleta migogoro ya muda mrefu katika nchi na jamii kwa ujumla.

Aidha, husababisha wawekezaji wa ndani na nje kuogopa kuwekeza jambo linaloathiri vibaya uchumi wa nchi na maendeleo ya watu. Siasa za uchochezi na hoja za chuki husababisha utulivu wa siasa kuporomoka na kuilazimisha serikali kutumia rasilimali kubwa na kuweka bajeti kubwa kwenye usalama badala ya kuwekeza katika huduma za jamii kwa wananchi kama afya na elimu.

Hali ya utulivu ikaharibika huchochea watu kutoshughulika na shughuli za kiuchumi na kijamii kwa ufasaha kwa kuwa hubaki kuhofia usalama wao, hivyo siasa za uchochezi na hoja za chuki huchelewesha maendeleo.

Kuharibu misingi ya maadili na uadilifu
Siasa za uchochezi na hoja za chuki hupunguza hoja za kweli na huzingatia matusi, uzushi na propaganda. Husababisha vijana kuiga mifano mibaya na kuamini mafanikio yanatokana na kuchochea au kugombanisha badala ya kufanya kazi kwa bidii na kwa uadilifu.

Siasa kama hizo si tu kwamba zinaharibu hali ya sasa, bali zinavunja misingi ya kesho na kulifanya taifa kupoteza dira, mshikamano na rasilimali muhimu kwa sababu ya migawanyiko isiyo na tija.

Kama taifa, tunapaswa kuchagua siasa za hoja, mshikamano na ujenzi wa pamoja. Ndipo wananchi wataweza kubeba mzigo wa taifa kwa moyo mmoja na taifa litapiga hatua. Athari za siasa za uchochezi na hoja za chuki wakati wa uchaguzi.

Kuvuruga amani ya taifa
Maneno ya chuki dhidi ya dini, makabila, ukanda au vyama huibua hisia za uhasama, maandamano ya vurugu, mashambulizi ya kisiasa au hata mapigano huweza kutokea.

Kugawa wananchi
Baada ya kuona taifa moja, wananchi hujigawa katika makundi yanayopingana kwa chuki. Pia, husababisha kushindwa kwa taifa kuungana baada ya uchaguzi, husababisha kudorora kwa maendeleo. Kudhofisha Imani kwa demokrasia Uchaguzi unapotawaliwa na kejeli, uzushi na matusi, husababisha wananchi kupoteza na kutotilia manani mchakato mzima wa uchaguzi.

Aidha, baada ya uchaguzi husababisha kushuka kwa ushiriki wa wananchi katika maamuzi ya kitaifa. Jinsi ya kupambana na siasa chafu na kujenga mshikamano wa kitaifa

Elimu ya uraia na amani
Kunatakiwa kutolewa elimu ya raia kuhusu haki zao na wajibu wao wakati wa uchaguzi na kuwaelimisha wananchi ukweli kuwa, tofauti za kisiasa si uadui, bali ni sehemu ya demokrasia.

Kusisitiza matumizi ya lugha ya heshima
Wanasiasa, viongozi wa dini, wanahabari na wananchi wote hawana budi kutumia lugha ya kujenga na si ya kubomoa.  Wanapaswa kukosoa hoja kwa heshima na si kwa matusi na kejeli.

Kukuza utambulisho wa kitaifa zaidi ya kufarakana
Kila raia akumbuke yeye ni Mtanzania kwanza kabla dini, chama au kabila lake. Pia, akumbuke na kuzingatia misemo kama ‘Nchi yetu ni hatima yetu.’

Hiyo iwe misingi ya kuimarisha mshikamano. Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii vihamasishe mshikamano Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii vinapaswa kuepuka kuchapisha, kutangaza au kusambaza taarifa za uchochezi, uzushi au lugha na hoja za chuki.

Wanaohusika kuandaa majukwaa ya midahalo wanatakiwa waandae hoja na mada zenye mwelekeo wa maendeleo, kutanguliza maslahi ya taifa, kuwaleta watu pamoja na si za kubomoa, kuwagawa watu katika makundi yanayopingana kwa maslahi binafsi.

Hao nao, wasiandae hoja chochezi na za chuki zinazosabisha uhasama katika miongoni mwa Watanzania. Viongozi na watu wengine wanaoeneza siasa za uchochezi na hoja za chuki kuwajibika kwa kauli zao. Sheria zichukue mkondo kwa wanaochechea chuki za waziwazi. Pia viongozi wa kisiasa waoneshe mfano kwa kujiepusha na siasa za kugawa taifa.

Wakati wa uchaguzi si wakati wa kugombana, bali ni wakati wa kushindana kwa hoja. Uchaguzi ni fursa ya kujenga taifa lenye demokrasia imara, mshikamano wa kweli na maendeleo endelevu. Tanzania ni yetu sote.
Amani, umoja na mshikamano wetu ni hazina tusivitupe kwa kauli za chuki au siasa za uchochezi.

Nchi yetu ni hatima yetu, taswira ya Tanzania iliyo bora ipo chini ya fikra za ubongo wetu na nguvu za mikono yetu.

Mwandishi ni msomaji na mchangiaji katika gazeti hili.

 

 

Habari Zifananazo

3 Comments

  1. I make over thirty k a month working part-time. I kept hearing from other people telling me how much money they could make online, so I decided to find out. Well, it was all true and it completely changed my life.

    This Is Where I Started……….www.get.money63.com

  2. I make over thirty k a month working part-time. I kept hearing from other people telling me how much money they could make online, so I decided to find out. Well, it was all true and it completely changed my life.

    This Is Where I Started……….www.get.money63.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button