ICC yawatia hatiani vigogo CAR

UHOLANZI: MAHAKAMA ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imewahukumu maafisa wawili wa zamani wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) kwa kuhusika na uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2013–2014.
Waziri wa zamani wa michezo, Patrice Edouard Ngaissona, aliyekuwa kiongozi wa wanamgambo wa Kikristo, amehukumiwa miaka 12 jela baada ya kupatikana na hatia katika mashitaka 28 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. SOMA: ICC kujadili waranti wanazotoa
Mbunge wa zamani na kamanda wa wanamgambo hao, Alfred Yekatom, maarufu kama “Rambo”, amehukumiwa miaka 15 jela kwa mashitaka 20, yakiwemo mauaji, mateso na vitendo vingine vya kikatili.
Mahakama ilibaini kuwa wawili hao waliongoza mashambulizi yaliyochangia mauaji ya raia na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu, wakati nchi hiyo ilipokuwa ikikabiliwa na machafuko makubwa.



