Tamasha nyimbo za dini kubadili vijana kimaadili

TAMASHA la uimbaji wa nyimbo za dini kwa vijana kutoka Makao Makuu ya Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria (DKMZV) mkoani Shinyanga imeeleza nia ya kuwabadilisha kimaadili vijana ili waweze kufikia malengo yao waliyoyakusudia.

Hayo yamesemwa na Nzinyangwa Mkiramwani ambaye ni Mratibu wa Tamasha la Twende kwa Yesu Ishi kwa Malengo kutoka Dayosisi hiyo inayojumuisha mikoa ya Shinyanga na Simiyu ambalo limefadhiliwa na Kampuni Jambo Group (JAMUKAYA) linalo tarajiwa kuanza rasmi tarehe 16,Agosti,2025.

Mkiramwani amesema tamasha hilo ni mara ya pili kufanyika ambapo yamekuwa yakitoa fursa kwa vijana kujifunza zaidi kimaadili kwa kupitia mahubiri ya neno la mungu nakuwafanya waelekee kule wanapo pataka.

“Kuna kwaya nane ambazo zitashiriki kutoa ujumbe na mahudbiri yanatarajiwa kutolewa na Mhashamu Askofu Jackson Sostenece sanjari na mchezo wa mbio za baiskeli ambao utakuwa kivutio kwa watu wengi nakuja kusikiliza neon la Mungu ”amesema Mkiramwani.

Katibu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria (DKMZV ) Happness Gefi amesema madhehebu yote wameyakaribisha kwa kuimba na vijana kuonyesha vipaji vyao kwani Dayosisi hii ina Majimbo 15 kati ya 28 yaliopo hapa nchini na tamasha lilianza rasmi kwenye Dayosisi ya Pwani inayojumuisha mikoa ya Pwani,Dar es –saalam na Zanzibar na limekwisha fanyika mara 12 hadi sasa.

Mratibu kutoka Ofisi ya Msaidizi wa Askofu wa Dayosisi hiyo Odolous Gyunda amesema mwaka jana walikuwa na tamasha kama hilo na walihudhuria watu zaidi ya 10,000 lakini sasa matarajio wawe zaidi sababu wameanza kulitangaza tamasha hilo mapema kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Msimamizi wa vipindi kutoka Jambo Media Renatus Kuluvia akiongea kwa niaba ya Msemaji wa Kampuni ya Jambo Group Nickson George amesema wamekuwa mstari wa mbele wakiendesha kipindi cha maudhui ya dini nakuona elimu wakaona haitoshi ni vyema wajumuike katika tamasha la nyimbo kwa kuendelea kuokoa kundi la vijana.

“ Tamasha hili ni maisha ya watu wote tunaweza kubadilisha utamaduni wetu kwa kanda ya ziwa kuwa ni nyimbo za injili kadri miaka inavyokwenda vijana nao wabadilike hoja zao ziwe kwenye misingi ya kidini”amesema Kuluvia.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button