Njaa yasababisha ukosefu wa amani

NEW YORK : KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameitaka jamii ya kimataifa kupinga vikali tatizo la njaa kama silaha ya vita, akisisitiza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa yanaathiri mavuno, usambazaji wa chakula na misaada ya kibinadamu.
Akihutubia kongamano la Umoja wa Mataifa kwa njia ya video, Guterres amesema migogoro inaendelea kuenea kutoka Gaza hadi Sudan na maeneo mengine, huku njaa ikichochea ukosefu wa utulivu na kudhoofisha jitihada za kudumisha amani duniani.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameonya kuhusu janga la njaa linalotishia maisha ya wakazi wa Gaza, wakati chakula cha misaada kikiisha na shinikizo la kimataifa likiongezeka kwa pande hasimu kusitisha mapigano ili kuruhusu operesheni kubwa ya misaada ya kibinadamu.
Wiki iliyopita, Mkurugenzi wa Kanda wa Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM), Othman Belbeisi, alisema Sudan inakabiliwa na moja ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu duniani, lakini limeendelea kusahaulika. SOMA: SUDAN: Tom Fletcher ataka hatua za haraka kukabiliana na mzozo



