Simba yadhaminiwa kwa Sh Bil.20

DAR ESSALAAM; KLABU ya Simba ya Dar es Salaam, imeingia mkataba wa udhamini wa Sh bil 20 kwa miaka mitatu na Kampuni ya Betway Afrika kuwa mdhamini mkuu wa klabu hiyo.

Hafla ya kutambulisha udhamini huo imefanyika leo jijini Dar es Salaam, ambapo Meneja Uendeshaji wa Betway Tanzania, Jimmy Masaoe, amewataka mashabiki wa klabu hiyo watarajie huduma bora kutoka kwao na zile walizobuni kwa ajili ya Simba.

Naye Mkuu wa Udhamini wa Betway Afrika, Jason Shield, amesema wameingia Simba kwa sababu ni timu kubwa Afrika na wamekuwa wakiifuatilia na wana furaha kufanikisha jambo hilo.

“Udhamini huu ambao thamani yake ni Sh Bilioni 20 kwa miaka mitatu, unaonesha namna Simba imedhamiria kuleta mabadiliko ya kuwa klabu kubwa,” amesema Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Simba, Zubeda Sakuru.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Muhene, amesema kazi yao ni ni kuhakikisha brand ya klabu inazidi kupanda siku baada ya siku.

“Nguvu kubwa ya Simba ni mashabiki wake ambao wanafanya wadhamini waje kuwekeza kwenye klabu yetu. Sisi tunataka Simba izidi kuwa na nguvu ndani na nje ya mipaka ya Tanzania,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button