Mwenyekiti mstaafu ateuliwa ubunge Missenyi

MISSENYI: Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi, Projestus Tegamaisho ameteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge wa Jimbo la Missenyi na wenzake saba.

Tegamaisho ambaye alikuwa mwenyekiti kwa miaka 10 amesema amepata uzoefu wa kila hitaji linalohitajika katika jimbo hilo na kudai kuwa ndio maana alichukua hatua za makusudi za kutangaza nia ya kugombea ubunge kwani anajua mahitaji halisi ya wananchi

Amesema serikali imefanya mambo makubwa katika kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati hivyo nia yake ni kujikita katika kubadilisha uchumi wa mwananchi mmoja mmoja ,kupunguza umasikini kwa ngazi ya kaya kupitia miradi ambayo itaishirikisha serikali na wadau wa maendeleo.

Tegamaisho atakumbukwa na waanchi na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi kwa ubunifu na uchapa kazi na ushawishi wa kukusanya mapato makubwa ya ndani hadi kufikia Sh bilioni 7 pamoja na kutumia fedha nyingi za mapato ya ndani kumaliza viporo vya maabara za sayansi katika jimbo hilo pamoja na kuwa kiunganisha kizuri kwa halmashauri nyingi nchini kuja kujifunza kutekeleza miradi kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button