Peskov: Hatulengi raia, tunataka amani

MOSCOW, URUSI : SERIKALI ya Urusi imedai kuwa Rais Vladimir Putin ana dhamira ya kweli ya kupatikana kwa amani kati ya nchi yake na Ukraine, licha ya mashambulizi ya hivi karibuni yaliyopelekea vifo vya watu 25, wakiwemo mjamzito na wafungwa 12.
Mashambulizi hayo yameripotiwa kulenga gereza lililoko mkoa wa Zaporizhzhia, eneo ambalo Urusi inadai ni sehemu ya ardhi yake. Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, ameyataja mashambulizi hayo kuwa ya makusudi na yaliyolenga maeneo ya kiraia.
Aidha, amesema shambulio la gereza hilo lilisababisha vifo vya watu 16 huku wengine wakijeruhiwa vibaya. Hii ni miongoni mwa matukio mengi ya mashambulizi yanayodaiwa kufanywa na Urusi katika kipindi cha mvutano unaoendelea.
Akijibu tuhuma hizo, Msemaji wa Kremlin, Dmitry Peskov, amesema jeshi la Urusi halilengi maeneo ya kiraia na kwamba nchi hiyo bado ina matumaini ya kupatikana kwa amani itakayozingatia maslahi yake. SOMA: EU yatangaza vikwazo vipya dhidi ya Urusi.
Kauli hiyo imetolewa saa chache baada ya Rais wa Marekani wa zamani, Donald Trump, kutoa shinikizo kwa Urusi kukomesha vita ndani ya siku 12 au ikabiliwe na vikwazo vipya.



