Matokeo kura za maoni UWT Manyara

MANYARA: Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri, amemtangaza Regina Ndege kuongoza kura za maoni za nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara baada ya kujizolea kura 891 kati ya zaidi ya kura 1000 zilizopigwa.
Pia alimtangaza Yustina Rahhi kushika nafasi ya pili Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Manyara kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya akupata jumla ya kura 703.
Katika uchaguzi huo uliowakutanisha wagombea nane kutoka wilaya za mkoa wa Manyara, mchuano huo wa kisiasa uliofanyika kwenye ukumbi mpya wa CCM Mkoa wa Manyara.
Chama Cha Mapinduzi kimeeleza kuridhishwa na utaratibu wa uchaguzi huo na kupongeza wajumbe kwa kuendesha mchakato kwa amani na ustaarabu
Anna Shinini kura 23
Scholar Molel 37
Paulina Nahato 71
Loema Peter 90
Joyclen Umbulla 168
Senorina Yunus 214
Rustina Rahh 703
Regina Ndege Qwaray 891

