Mashambulizi Kiev yaua watu 31

KIEV, UKRAINE : IDADI ya watu waliouawa katika jiji la Kiev, Ukraine, imeongezeka na kufikia 31 kufuatia shambulio la makombora la Urusi. Mamlaka zimesema miili zaidi imeopolewa kutoka chini ya vifusi vya majengo yaliyoharibiwa.

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, amesema kuwa Urusi ilitumia zaidi ya droni 3,800 na makombora 260 mwezi Julai pekee kushambulia maeneo mbalimbali nchini humo. Amesisitiza kuwa mashambulizi hayo yanaweza kusitishwa iwapo jumuiya ya kimataifa itachukua hatua za pamoja.

Hatahivyo, Ujerumani imetangaza kuwa itawasilisha kwa Ukraine mifumo miwili ya ulinzi wa anga ya kisasa ya Patriot kutoka Marekani, ikiwa ni sehemu ya msaada wa kuimarisha ulinzi wa anga ya nchi hiyo. SOMA: Zelensky: Mali za Urusi Zitaifishwe

 

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I am making a good salary from home $4580-$5240/week , which is amazing under a year ago I was jobless in a horrible economy. I thank God every day I was blessed with these instructions and now its my duty to pay it forward and share it with Everyone, Here is I started_______ https://Www.Workapp1.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button