Simba, Yanga zashindana kushusha vyuma!

DAR ES SALAAM; MIAMBA ya soka nchini Simba na Yanga inaendelea kushindana katika kutangaza wachezaji wapya ziliowasajili kwa msimu ujao wa mashindano mbalimbali.

Leo saa moja usiku walianza Simba walipotambulisha usajili mpya wa mshambuliaji raia wa Ghana Jonathan Sowah, aliyejiunga na miamba hiyo akitokea Singida Blackl Stars, alikomaliza msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa na mabao 13 baada ya kusajiliwa dirisha dogo.

Saa tatu na nusu usiku ilikuwa zamu ya Yanga nayo ilipotambulisha usajili wa Celestine Ecua raia wa Ivory Coast, aliyechezea Asec Mimosas ya Ivory Coast kwa mkopo akitokea Zoman FC. Nyota huyo  amekuwa Mchezaji Bora wa ligi msimu wa mwaka 2024.25.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button