Wazazi wafundwa matumizi ya teknolojia kwa vijana

SHINYANGA: Wazazi mkoani Shinyanga wameshauriwa kutochoka kufundisha matumizi mazuri ya teknolojia yanayoendelea kuwepo na kuepukana na matumizi ya dawa ya kulevya kwa vijana.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Rocken Hill na Anderlek Ridgesi liyopo Manispaa ya Kahama, Alexander Kazimil amesema hayo leo Agosti 6, katika mahafali ya 21 ya darasa la saba na mahafali ya 17 ya kidato cha nne huku akieleza mtoto akimaliza kidato cha nne sio kumuachaniza kwa madai amekuwa bila kumkumbushia maadili na malezi mema.

Kazimil amesema teknolojia ni nzuri pia mbaya haiwezi kukwepeka kwa watoto hivyo jitihada zinahitajika kwa wazazi,walimu na jamii nzima kuhakikisha watoto wanapata malezi na kuwakumbusha kila siku kutotumia madawa ya kulevya.
“Muwaeleze watoto kuwa wavumilivu kwani maisha yanaweza kuwa juu au chini nakutambua vipaji walivyonavyo ambavyo vitawasaidia kujipatia ajira na kuendeleza maisha yao,”amesema Kazimil.
Kazimil amesema vijana wanatakiwa kuandaliwa kiimani na kimaadili kwani wapo wazazi wengine wamekuwa wakilea watoto wao kama mabosi kwa kuogopa hata kuwatuma kazi majumbani kwani wakifanya hivyo wataweza kutengeneza kizazi kisicho bora hapo baadaye.

Kazimil amesema elimu siyo ya kuchezea na kwani ndiyo inayoendesha maisha haimuondolei mtu umasikini bali inamtaka kila mmoja kujifunza na kupambana na wimbi la umasikini.
Mkurugenzi wa Shule za msingi Rocken Hill Zephania Madaha alisema shule hizo zinawahitimu 186 wa darass la saba zimekuwa zikifundisha masuala ya Mshikamano,maadili na imani kwani wameona dunia inavyokwenda na kuwataka wawe na hofu ya mungu ili waweze kutimiza ndoto zao.

Naye Mkurugenzi wa shule ya Anderlek Ridges Godwin Ng’osha amesema wamekuwa wakifanya viziri kitaaluma nakuwapongeza wazazi kwa kuwaamini kuwa na watoto wao muda wote kwa kipindi cha miaka minne
Mgeni rasmi katika mahafali hayo katibu wa baraza la ushauri la wazee. Anderson Lyimo amesema watoto wasipolelewa vizuri watamomonyoka kimaadili nakuwa taifa la watu wa hovyo hivyo mafundisho mema yaendelee ndani ya familia ili nchi iwe ya amani na utulivu hasa kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu.



