Sudan yalia na mlipuko wa kipindupindu

GENEVA: SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa takribani watu 100,000 nchini Sudan wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu tangu mwezi Julai mwaka jana.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema Sudan inakabiliana na changamoto kubwa ikiwemo baa la njaa na mlipuko wa magonjwa mbalimbali, huku kipindupindu kikiendelea kusambaa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. SOMA: UMMY :Mikoa miwili bado ina kipindupindu
Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa Umoja wa Mataifa (ACANU) uliofanyika mjini Geneva, Dk. Ghebreyesus alisema kampeni za chanjo dhidi ya kipindupindu zimefanyika katika majimbo kadhaa, ikiwemo mji mkuu wa Khartoum, ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.



