Nguli wa mitindo Miriam Odemba azindua kitabu maendeleo ya mitindo
Nguli wa mitindo Miriam Odemba amezindua kitabu cha kuhamasisha maendeleo ya mitindo tukio lilofanyika jana usiku Dar es Salaam

DAR ES SALAAM: MWANAMITINDO nguli wa kimataifa, Miriam Odemba, amezindua kitabu chake kipya kinacholenga kuhamasisha maendeleo ya sekta ya mitindo na urembo nchini.
Miriam ameeleza dhamira yake ya kuwawezesha vijana na chipukizi kufanikisha ndoto zao katika tasnia hiyo.
Akizungumza jana Agosti 10, 2025 katika hafla ya uzinduzi, Miriam alisema kitabu hicho ni matokeo ya miaka mingi ya uzoefu na mafanikio katika mitindo ya kimataifa, na kinawakilisha watu wote wanaoamini katika ubunifu na urembo.
“Ninapenda sana mitindo, na natamani wengi wapende na kufanikiwa zaidi kama mimi. Humu nimeweka wazi siri mbalimbali za kuwa juu katika urembo na mitindo. Ni hazina na faida kwa taifa zima,” alisema Miriam.
Mwonekano wa nje kitabu alichozindua jana Miriam Odemba.
Hafla hiyo ilihusisha pia tamasha maalumu lililopewa jina la “Sauti ya Mitindo”, lililowakutanisha mabingwa na chipukizi wa mitindo kutoka maeneo mbalimbali ya nchi. Wadau wa sekta hiyo walijadili fursa na changamoto zinazokabili tasnia ya mitindo, urembo na fashion nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa BASATA, aliyeshindwa kuhudhuria hafla hiyo kutokana na majukumu maalum ya serikali, mwakilishi huyo alisema kuwa Katibu Mtendaji, Kedmond Mapana, alitamani sana kuwepo na alifuatilia kwa makini tukio hilo. Aidha, aliunga mkono juhudi za tamasha hilo akisema ni endelevu na ni hazina kwa taifa katika tasnia ya urembo na mitindo.
“Ninamwakilisha Katibu Mtendaji, Kedmond Mapana, ambaye alitamani sana kuwepo leo, na anakupongeza sana Miriam kwa hatua hii kubwa. Anasema kuwa unaipeperusha vyema bendera ya nchi yetu kimataifa bila kuchoka, na sisi kama BASATA tumekuandalia kitu kizuri ambacho tutakitangaza kuanzia Jumatatu,” alisema mwakilishi huyo.
Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) pia lilimpongeza Miriam kwa mchango wake mkubwa wa kuiwakilisha vyema Tanzania kimataifa na kuchochea mabadiliko chanya katika tasnia hiyo.
Katika tukio la kusisimua, binti mwenye umri wa miaka 11, Sofia, alishindwa kuzuia machozi baada ya kumpanda jukwaani kumshukuru Miriam kwa kumsaidia kuhudhuria hafla hiyo bila malipo.
“Nilimsikia Miriam akiongelea kuhusu tamasha la mitindo kwenye redio ya Clouds, katika kipindi cha ‘Leo Tena’. Niliguswa sana na kumwambia mama tumpigie simu. Mama yangu anajua kuwa ninapenda mitindo, na fedha pekee tuliyokuwa nayo ilikuwa ni shilingi elfu moja ya vocha. Baada ya mama kukubali na kumpigia Miriam, siamini kuwa leo hii nimehudhuria tukio hili la kipekee…” alishindwa kuendelea kusema na kuangusha machozi ya hisia.
Runway ya uzinduzi ilifanywa na vijana kutoka makundi maalum ya Salvation Army jijini Dar es Salaam, ikiwemo watoto waliojishughulisha na fashion show ya awali. Jukwaa hilo limepewa hadhi ya kimataifa, jambo lililowagusa wadau na kuchangia zaidi ya Shilingi milioni 1.2 kwa ajili ya mfuko wa kusaidia watu wenye mahitaji maalumu.
Miriam amejulikana kwa jitihada zake katika kusaidia wasiojiweza, ikiwa ni pamoja na msaada wa karibuni kwa akina mama na watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Kwa jumla, mamodeli 13 walishiriki kwenye runway hiyo, wakiwa wamevalia mavazi ya kipekee yaliyoundwa na wabunifu nguli nchini, wakiwemo wakufunzi kutoka Anna Collection, pamoja na ofisi za wabunifu maarufu Hamissa Mobetto Stylish na Mike Stylish.
Your articles always leave me thinking.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… Y You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
For details check ——-⫸ http://Www.EarnApp1.Com