Mali yakabili jaribio la mapinduzi

BAMAKO , MALI : SERIKALI ya kijeshi nchini Mali imewakamata karibu wanajeshi 50 wanaoshukiwa kupanga njama ya kupindua utawala huo, ambao wenyewe ulipata madaraka kupitia mapinduzi.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP limeripoti kuwa miongoni mwa waliokamatwa ni Jenerali Abass Dembele, Gavana wa zamani wa Jimbo la Mopti na afisa wa kijeshi anayeheshimika nchini humo. SOMA: Wapinzani 11 waachiliwa huru -Mali
Tangu kuchukua madaraka mwaka 2021, utawala wa kijeshi wa Mali umekuwa ukikosolewa kwa kuendeleza ukandamizaji dhidi ya wakosoaji, hususan wale wanaoupinga kutokana na kushindwa kushughulikia machafuko yanayochochewa na makundi ya itikadi kali katika Kanda ya Sahel.



