MALI: MAHAKAMA moja nchini Mali imewaachilia huru wapinzani 11 waliokamatwa kwa tuhuma za kula njama dhidi ya mamlaka za nchi, baada ya kutoa wito wa kurejesha utawala wa kiraia.
Miongoni mwa watu walioachiliwa huru ni mawaziri wa zamani, viongozi wa vyama vya siasa na asasi za kiraia ambao mwezi Machi walisaini tamko la kulitaka jeshi kurejesha madaraka kwa raia.
Watu hao walikamatwa mwezi Juni kwa kula njama dhidi ya mamlaka halali na kufanya mkutano haramu, wakati walipokutana kwenye nyumba ya mmoja wao mjini Bamako.
Taifa hilo la magharibi mwa Afrika limekuwa katika mizozo ya kisiasa na kiuchumi kadhalika na ghasia za makundi ya watu wenye silaha tangu mwaka 2012. SOMA: Waziri mkuu mali avuliwa madaraka
Mnamo mwezi Juni 2022, utawala wa kijeshi ulitangaza kwamba ungerejesha serikali ya kiraia mwishoni mwa mwezi Machi 2024 lakini mpaka sasa utawala wa kiraia bado haujafanikiwa.