Karia athibitishwa urais TFF hadi 2029

TANGA; MKUTANO Mkuu wa Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), asubuhi hii umemthibitisha Wallace Karia kuwa Rais wa shirikisho hilo kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Hatua ya kumthibitisha imetokana na kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo, hivyo wajumbe wote 76 waliokuwa na sifa ya kupiga kura walinyoosha mikono kumthibitisha kwa wadhifa huo hadi mwaka 2029.

Awali Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Kiomoni Kibamba aliwajulisha wajumbe kuwa kwa vile Karia alikuwa mgombea pekee angepewa dakika za kujieleza kisha mkutano umthibitishe.-

Hata hivyo Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Murtaza Mangungu ambaye ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, alisimama na kutoa hoja ya kutaka athibitishwe kwanza na kama ana maelezo atasema baada ya kuthibitishwa, kauli ambayo iliungwa mkono na wajumbe wote.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button