Putin, Zelensky wakubaliana kukutana

WASHINGTON DC: MARAIS wa Urusi na Ukraine wamekubaliana kufanya mazungumzo ya amani, hatua ambayo ni ya kwanza tangu Urusi iivamie Ukraine zaidi ya miaka mitatu iliyopita.
Mkutano huo umepangwa kufanyika baada ya mazungumzo marefu yaliyofanyika jana mjini Washington, Marekani, yakihusisha Rais Donald Trump na viongozi kadhaa wa mataifa ya Ulaya.
Baada ya kikao hicho kilichofanyika Ikulu ya White House, Rais Trump alipiga simu kwa Rais Vladimir Putin wa Urusi na kukubaliana naye kuhusu umuhimu wa kuitisha mazungumzo ya ngazi ya juu kati ya Urusi na Ukraine.
Kwa upande wake, Rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine alisema yuko tayari kukutana na Putin. Aidha, alimshukuru Trump pamoja na viongozi wa Ulaya kwa kuongoza jitihada za kumaliza vita vinavyoendelea nchini mwake. SOMA: Marekani yakanusha kusitisha silaha Ukraine



