SADC yawafunza Watanzania 100 uangalizi uchaguzi nchi wanachama

DAR ES SALAAM; JUMUIYA ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) imeanza kutoa mafunzo kwa wadau 100 wa uchaguzi nchini yakilenga kuwawezesha kushiriki katika Misheni ya Uangalizi wa Uchaguzi ya SADC (SEOMs) katika uchaguzi mkuu wowote unaofanyika katika nchi wanachama.

Mafunzo hayo ya siku tano yalifunguliwa jana Dar es Salaam na Mjumbe wa Tanzania katika Baraza la Masuala ya Uchaguzi la SADC (SEAC), Jaji mstaafu Dk Fauz Twaib.

Dk Twaib alisisitiza umuhimu wa kuwa na waangalizi wa uchaguzi wenye mafunzo bora katika kuimarisha demokrasia na utawala bora ndani ya SADC yenye nchi wanachama 16.

“Mafunzo haya yanalenga kuwawezesha kuwa na ujuzi, maarifa na zana muhimu ili muweze kuangalia uchaguzi mkuu wowote unaofanyika katika nchi wanachama za SADC,” alisema Dk Twaib.

Aliwaeleza washiriki, ambao ni pamoja na maofisa wa serikali, wawawakilishi wa jamii na wataalamu wa masuala ya uchaguzi.

“Ni sehemu ya juhudi za kanda za kuimarisha demokrasia na utawala mwema, mtatumwa katika nchi za SADC ili kushuhudia jinsi wapigakura wanavyotekeleza haki zao za kidemokrasia kuchagua viongozi wao,” alisema.

Mafunzo hayo yameandaliwa kwa ushirikiano wa Sekretarieti ya SADC, SEAC, Taasisi ya Uchaguzi kwa Demokrasia Endelevu barani Afrika (EISA) na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya Tanzania.

Alisisitiza kuwa uelewa mzuri wa kanuni na miongozo hiyo ni muhimu kwa waangalizi ili kuwapa taswira sahihi ya kufuatilia utekelezaji wa nchi wanachama.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button