Binti wa Kimara ang’ara mnada wa Piku

DAR ES SALAAM; Binti wa miaka 25 kutoka Kimara Baruti jijini Dar es Salaam, Jenipher Ayubu ameshinda bidhaa kwenye minada mitatu yenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni moja kupitia jukwaa jipya la kidigitali la Piku.
Jukwaa la Piku limeanzishwa kwa lengo la kutoa fursa kwa wananchi kujikwapulia bidhaa za thamani kwa gharama nafuu kwa njia ya mnada wakipeke ambapo dau dogo na la kipeke hushinda mnada huo.
Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi Ayubu amesema: “Nilichotumia ni fedha ndogo tu, kitu cha ajabu ni kwamba sikuwa naamini kama kweli naweza kushinda.
“Lakini leo leo nimeletewa bidha zangu, bada ya jana usiku kupata ujumbe kuwa dau zangu zote tatu zimekuwa ndogo na za kipekee. Najivunia kuwa sehemu ya washindi wa Piku,” amesema Ayubu.
Amesema ndoto yake muda mrefu ni kumiliki saa aina ya Coach pamoja na pafyumu ya Jean Paul Gaultier Le Male Elixir na kwamba sasa ndoto yake imetimia.



