Mauaji mapya ya waasi yatikisa Colombia

COLOMBIA : NCHINI Colombia , watu 18 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 40 wamejeruhiwa baada ya kushambuliwa na kundi la waasi.
Akizungumzia kuhusu tukio hilo nchini Colombia, Rais Gustavo Petro amesema makundi yaliyokataa makubaliano ya amani ya mwaka 2016 ndiyo yanayohusika. Katika mji wa Cali, gari lililobeba vilipuzi lililipuka karibu na kambi ya jeshi la anga na kuua watu sita huku 71 wakijeruhiwa.
Hapo awali, helikopta ya polisi ilidunguliwa kwenye eneo la Amalfi na kuua maafisa 12. Machafuko hayo yamekuwa yakiendelea kwa miongo kadhaa na kusababisha vifo vya zaidi ya nusu milioni. SOMA: Mgombea Urais Colombia afariki dunia



