Israel kushika usukani Gaza – Netanyahu

ISRAEL: WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amesema serikali yake itachukua udhibiti kamili wa mji wa Gaza. Amesema hatua hiyo itaambatana na masharti ya mazungumzo na Hamas kuhusu kuachiliwa kwa mateka wa Israel.

Operesheni hiyo inatarajiwa kuanza katika siku chache zijazo. Wakati huohuo, takwimu mpya zinaonyesha asilimia 83 ya waliouawa huko Gaza hadi Mei 2025 walikuwa raia. Ripoti ya mashirika manne ya habari imeeleza kuwa idadi ya raia waliopoteza maisha ni kubwa kuliko ilivyodaiwa na jeshi la Israel.

Jeshi hilo limekuwa likisema idadi ya raia wanaouawa ni ndogo mno ikilinganishwa na wapiganaji. SOMA: UN yaipinga Israel kuongeza mapigano Gaza

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button