WHO: Joto kazini ni tishio la afya

MAREKANI : SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) wamesema mamilioni ya wafanyakazi dunia wamekuwa wanakumbana na hali ya joto kali wakiwa makazini na kuahatrisha afya zao .
Ripoti hiyo imeziomba mamlaka mbalimbali za serikali , waajiri na wafanyakazi duniani kushirikiana kuandaa mikakati madhubuti ya kukabiliana na tatizo hilo. Hii itakuwa ni mara ya kwanza tangu 1969 kwa WHO kutoa ripoti mahsusi kuhusu joto kazini.
Mkurugenzi wa mazingira na afya wa WHO, Rüdiger Krech, amesema ugunduzi wa ripoti hiyo unatoa muongozo wa dunia kuanza kuchukua hatua kudhibti athari za mabadiliko ya tabianchi . SOMA: Joto kali Ulaya laua watatu



