Ndoiyo akabidhiwa fomu Ngorongoro

OFISI ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ngorongoro imetoa fomu ya uteuzi kwa mgombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Ngorongoro, Yannick Ndoiyo
Ndoinyo ameishukuru Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi,wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro kwa imani kubwa walionesha kwake kugombea nafasi hiyo ya ubunge na kuahidi kusimamia sekta za utalii,mifugo,elimu na afya pamoja na kusimamia sera za Chama cha Mapinduzi ili wananchi wapate huduma bora kwa ustawi wa Jkamiii ya wana Ngorongoro
Pia ameishukuru Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi inayoongozwa na Emmanuel Mchome kwa ushirikiano na ukarimu waliyompatia katika hatua hiyo muhimu ya kuchukua fomu ya uteuzi kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 mwaka huu



