Dk Nchimbi: Matiko ni silaha madhubuti kisiasa

MARA; MGOMBEA Mwenza wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel Nchimbi amesema chama hicho kimepata silaha madhubuti ya kisiasa kwa kumpata Esther Matiko kugombea ubunge wa Jimbo la Tarime Vijijini, kutokana na uzoefu wake na uwezo mkubwa wa kujenga hoja bungeni.

Akihutubia mkutano wa hadhara juzi jioni katika Chuo cha Ualimu Buhemba, wilayani Tarime, Nchimbi alisema Matiko amekuwa miongoni mwa wanasiasa wachache wa mkoa wa Mara wanaotambulika kitaifa kwa ushawishi na msimamo thabiti, hivyo CCM imepata mwakilishi atakayehakikisha sauti za Wanatarime zinasikika ipasavyo bungeni.

“Natamka mbele yenu, hakuna mtu mwenye shaka na uwezo wa Esther Matiko. Yeye ni miongoni mwa wabunge waliowahi kutambulika kwa kujenga hoja, kufanya uchambuzi na kutetea anachokiamini. Sasa kwa kuwa yupo CCM, Tarime mmepewa mwakilishi wa kweli wa kuwazungumzia bungeni na kuwasemea,” alisema Nchimbi.

Habari Zifananazo

One Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button