Komandoo Kalala kuja na kibao kuhamasisha vijana uchaguzi

DAR-ES-SALAAM : KIJIWENI leo tunakutana na mkongwe wa muziki wa dansi, Komandoo Hamza Kalala akiwa kwenye Kituo cha Runinga cha UTV na gitaa lake.

Huku akicharaza kamba za gitaa lake anatoa ujumbe kwa vijana kushiriki kwenye kampeni za uchaguzi za vyama vyote ili wapate uzoefu wa kusikiliza sera mbalimbali za wagombea na kuamua ifikapo Oktoba 29, 2025.

Anasema umuhimu wa kusikiliza sera za wagombea wote ni fursa ya kuepuka ulaghai wa kisiasa wa baadhi ya vyama na wagombea wake na pia ni fundisho kuwa vijana si miliki ya chama fulani bali ni kundi linalojitambua lenye dhima kubwa katika uongozi wa taifa.

“Nawasihi vijana wahudhurie mikutano ya kampeni ya vyama vyote na kusikiliza sera zao ili ziwaongoze katika kufanya maamuzi siku ya hukumu,” aliongeza mwanamuziki huyo. SOMA : KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025: Kataa siasa za uchochezi, hoja za chuki

Anasema yeye binafsi atawasikiliza wagombea wote na mwisho wa siku anaamini atampigia kura mgombea wa chama chenye sera bora zenye maslahi na taifa na zinazotekelezeka.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button