Msigwa: Samia amefanya maajabu

NYAMAGANA : KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Peter Msigwa amesema mgombea urais wa Tanzania kupitia chama hicho, Samia Suluhu Hassan amefanya maajabu katika miaka minne ya kuiongoza nchi. Msigwa alisema hayo kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa urais kupitia CCM katika eneo la Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara.

Alisema miradi ya maendeleo, nidhamu ya kiuongozi na mageuzi ya sekta mbalimbali vimeonesha taswira mpya ya Tanzania inayojengwa juu ya misingi ya huruma, maarifa na weledi. “Wakati ule nikiwa kule nilikotoka (Chadema) tulidhani miradi mingi itakwama, tuliona kama Samia kwa kuwa ni mwanamke hataweza kusimamia taifa.

Lakini ndugu zangu, amefanya maajabu makubwa. Leo tunashuhudia miradi mikubwa ikikamilika kwa kasi, nidhamu kubwa imewekwa serikalini na kila sekta imeguswa na uongozi wake,” alisema Msigwa. Alisema ruzuku za mbolea zimefungua njia mpya ya wakulima wa Tarime na nchi nzima kushiriki kwenye utajiri unaotokana na kilimo.

“Asilimia kubwa ya wananchi wa Tarime ni wakulima wa kahawa, mahindi na ulezi. Samia amepandisha ruzuku, ameimarisha miundombinu na amewaweka wakulima katika nafasi ya kuwa mabilionea wa kesho.

Tafiti za World Economic Forum zinaonesha utajiri mpya utatokana na kilimo na ilani ya CCM inamuandaa Mtanzania kushiriki kikamilifu,” alisema Msigwa. Alisema mafanikio hayo si ya kawaida na ni uthibitisho wa dhamira ya kweli ya Rais Samia ya kumkomboa Mtanzania kutoka kwenye umasikini.

“Kazi aliyoifanya Samia nchi nzima ni ya kihistoria na yenye alama za maajabu. Uchaguzi huu ni nafasi ya kuthibitisha kuwa Watanzania tunaunga mkono dhamira yake, mipango yake na nia yake ya kweli ya kuondoa umasikini na kuijenga Tanzania yenye fursa,” alisema.

Alisema CCM ni chama chenye sera makini na viongozi wenye maono hivyo kura kwa chama hicho zitaendeleza maajabu ya Rais Samia. SOMA: Msigwa kunguruma Iringa Ijumaa

Habari Zifananazo

3 Comments

    1. I make $88 an hour to work part time on a laptop. I never thought it was possible but my closest friend easily made $18,000 in 3 weeks with this top offer and she delighted me to join. .Visit the following article for new information on how to access…….
      .
      HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  1. Burkina Faso bans homosexuality as a crime punishable with prison, fines

    In the new law, those found guilty of homosexuality could face a two- to five- year prison sentence.

    Burkina Faso President Ibrahim Traore.
    Burkina Faso President Ibrahim Traore arrives to the Grand Kremlin Palace in Moscow, Russia, on May 10, 2025 [Stanislav Krasilnikov/RIA Novosti via AP]
    Published On 2 Sep 2025
    2 Sep 2025

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button