Makalla akagua uwanja wa AFCON , ujenzi wafikia 60%

ARUSHA: MKUU wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, leo Ijumaa Septemba 5, 2025 ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu unaojengwa na Serikali kwa gharama ya Shilingi Bilioni 340 katika Kata ya Olmot, Jijini Arusha. Uwanja huo unatarajiwa kutumika kwenye mashindano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2027.

Ukaguzi huo umefanyika baada ya kikao kazi kilichoshirikisha wakuu wa idara na mamlaka zinazohusika na miundombinu ya maji, nishati, barabara na mawasiliano katika eneo la mradi. Kikao hicho kimeazimia kuunda kikosi kazi cha wataalamu kutoka sekta hizo, kitakachoongozwa na mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ambao watakuwa uwanjani muda wote kusimamia utekelezaji wa mpango mkakati wa dharura wa miundombinu hiyo. SOMA: Miundombonu ya michezo miaka 4 ya Dk Samia

“Kama Mkoa wa Arusha tunajivunia utalii. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mawili makubwa kupitia Royal Tour ametangaza utalii, na sasa ametuletea utalii wa michezo (sport tourism). Uwepo wa uwanja huu utaongeza mzunguko wa fedha, kuchochea ukuaji wa biashara na uchumi wa mtu mmoja mmoja pamoja na Mkoa kwa ujumla.Tunamhakikishia Rais kuwa tutamuwakilisha vyema kwa kusimamia ukamilishaji wa uwanja huu, na mkandarasi ametuthibitishia kwamba utakamilika ifikapo Julai 2026,” amesema Makalla.

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button