Waziri Mkuu Japan atangaza kujiuzulu

TOKYO, JAPAN: WAZIRI Mkuu wa Japan, Shigeru Ishiba, ametangaza kujiuzulu jana jioni baada ya kushika wadhifa huo kwa chini ya mwaka mmoja. Hatua hiyo imekuja kufuatia kupoteza uungwaji mkono ndani ya Chama cha Liberal Democratic (LDP) na kushindwa kudhibiti wingi wa viti katika mabunge yote mawili.
Ishiba, ambaye aliongoza serikali tangu Oktoba mwaka jana, alisema ataendelea kushika majukumu yake hadi chama chake kitakapomteua kiongozi mpya. “Sasa ndiyo wakati sahihi wa kujiuzulu,” alisema kiongozi huyo, akisisitiza dhamira yake ya kuhakikisha mpito wa uongozi unafanyika kwa utulivu.
Tangazo hilo limefanyika muda mfupi baada ya Japan kukamilisha makubaliano ya kibiashara na Marekani. Serikali ya Ishiba iligeuka kuwa ya wachache baada ya muungano wa LDP na chama kidogo cha Komeito kupoteza wingi wa viti katika baraza la juu mwezi Julai, hali iliyoongeza shinikizo dhidi ya uongozi wake. SOMA: Majaliwa akutana na Waziri Mkuu wa Japan



