Labour yashinda uchaguzi, Støre abaki madarakani

OSLO, NORWAY : WAZIRI Mkuu wa Norway, Jonas Gahr Støre ametangaza ushindi katika uchaguzi wa bunge uliofanyika jana Jumatatu. Støre, ambaye anaongoza Chama cha Labour, amesema ushindi huo umetokana na chama chake kuibuka cha kwanza kwa kupata takribani asilimia 28 ya kura, huku akisaidiwa na vyama vingine vinne vya mrengo wa kushoto vilivyomuunga mkono.

Kwa mujibu wa matokeo hayo, Støre ataendelea kuiongoza Norway kwa muhula mwingine wa miaka minne. Hata hivyo, uchaguzi huo pia ulishuhudia ongezeko kubwa la uungwaji mkono wa chama cha kizalendo cha Progress, kinachopinga uhamiaji. Chama hicho kimekuwa cha pili kwa ukubwa bungeni, jambo linaloibua wasiwasi mpya wa kisiasa nchini humo.SOMA: Zanzibar, Norway kuimarisha ushirikiano

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button