Viwanja vipya kuibua vipaji Zanzibar

ZANZIBAR : RAIS wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali inaendelea na mageuzi makubwa ya michezo kwa kujenga na kukarabati viwanja vya kisasa ili kukuza vipaji, kuandaa wataalamu na kuiandaa Zanzibar kushiriki mashindano ya kimataifa ikiwemo AFCON 2027.

Dk. Mwinyi alitoa kauli hiyo alipofungua kiwanja kipya cha michezo cha kisasa kilichopo Kitope, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Septemba 9, 2025. Amesema tayari ukarabati wa viwanja vya Amani Complex, Mao Tse Tung na Gombani umekamilika, huku viwanja vipya vikijengwa Kizimkazi (viti 21,000), Fumba (viti 31,000) pamoja na viwanja 17 vya mikoa na wilaya.

Aidha, Dk. Mwinyi alibainisha kuwa michezo ni nyenzo muhimu ya kuibua vipaji, kutoa ajira, kukuza utalii na kudumisha utamaduni, sambamba na kuhakikisha ushiriki wa vijana, wanawake na makundi maalum katika mazingira rafiki na salama. SOMA: Uwanja wa kisasa wakamilika Zanzibar

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button