WHO : Tutaendelea kubaki Gaza

GENEVA,USWISI: SHIRIKA la Afya Duniani (WHO) limesema wafanyakazi wake wataendelea kubaki katika Jiji la Gaza licha ya Jeshi la Israel kuwataka watu kuondoka katika Ukanda wa Gaza.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus, alisema Jumatano Septemba 10, kuwa shirika hilo limefadhaishwa na agizo hilo la kuwataka watu zaidi ya milioni moja kuhamia kwenye kile kinachoitwa na Israel eneo salama la kibinadamu.

“Zaidi ya nusu ya hospitali zinazofanya kazi Gaza zipo ndani ya jiji, na eneo hilo haliwezi tena kupoteza vituo zaidi vya afya,” alisema Ghebreyesus. SOMA: Israel yaamuru wakaazi Gaza kuondoka

Msimamo huo umetolewa wakati Israel ikiendeleza mashambulizi ya kuyabomoa majengo makubwa mjini humo ikidai ni vituo vya mawasiliano na mashambulizi vya Hamas.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button