Putin: Msitumie Mali za Urusi

MOSCOW, URUSI : SERIKALI ya Urusi imeonya kuwa italishambulia taifa lolote la Ulaya litakalothubutu kuchukua mali zake zilizozuiwa, kufuatia mapendekezo ya Umoja wa Ulaya (EU) ya kutumia fedha hizo kufadhili ulinzi wa Ukraine.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, ameziagiza nchi wanachama kutafuta mbinu mpya za kusaidia Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi, ikiwemo kutumia mali za Urusi zilizozuiwa barani Ulaya.
Marekani na washirika wake tayari walizuia mali zinazokadiriwa kufikia dola bilioni 350, ikiwemo za wafanyabiashara, Wizara ya Fedha ya Urusi na Benki Kuu ya nchi hiyo. Urusi imepinga vikali hatua hiyo na kuitaja kuwa ni wizi, ikilalamikia matumizi ya faida zinazotokana na malipo ya riba kwa mali zake. SOMA: Zelensky: Mali za Urusi Zitaifishwe