Kivuko MV Bukondo chazinduliwa Mwanza

MWANZA : KIVUKO cha MV Bukondo s  kinachotarajiwa kufanya safari zake katika visiwa vya ziwa Victoria, wilayani Ukerewe mkoani Mwanza kimeshushwa kwenye maji leo Septemba 16, 2025 baada ya ujenzi wake kukamilika.

Ni kimoja kati ya vivuko vitano vya serikali vinavyojengwa katika karakana ya Songoro Marine, wilayani Ilemela (Mwanza) kwa gharama ya takribani Sh billioni 28. “Nipo hapa kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Mwanza kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi huu.

“Vivuko ni muhimu kwasababu asilimia 53 ya mkoa wa Mwanza ni maji ya ziwa Victoria. Kwahiyo shughuli za usafirishaji ni kipaumbele cha serikali yetu kuhakikisha wananchi wanaondokana na adha ya usafiri, ”amesema mkuu wa Mkoa, Said Mtanda wakati wa uzinduzi wa kivuko hicho.

Amefafanua kwamba ujenzi wa  vivuko vingine vinne uko hatua za  mwisho, na bado serikali ina mpango wa kujenga vingine zaidi ili kukidhi mahitaji ya wananchi wote wanaoishi katika visiwa mbalimbali. Kadhalika hatua hiyo itapunguza  ajali ziwa Victoria, kwani usafiri sasa utakuwa wa uhakika wakati wote, amesema.

Mwenyekiti Chama Cha mapinduzi Mkoa, Michael Lushinge, alitoa pongezi kwa serikali na mkandarasi, akasema ujenzi kutekelezwa na wazawa ni hatua kubwa kimaendeleo kwani mzunguko wa fedha unasalia hapa hapa nchini. SOMA: Bil 3.8/- kujenga kivuko Mwanza

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button