Maelfu ya wafanyakazi waandamana Paris

PARIS: MAELFU ya wafanyakazi mjini Paris wamegoma kufanya kazi na kuandamana jijini Paris wakipinga mpango wa serikali wa kupunguza bajeti.

Waandamanaji hao wakiwemo walimu, madereva wa treni, wafamasia, wahudumu wa hospitali na vijana wa shule za sekondari, wamesema hatua hiyo inalenga kushinikiza serikali kuangalia upya sera za kifedha ili kulinda maslahi ya taifa.

Vyama vya wafanyakazi vinaitaka serikali kufuta mpango wa kifedha ulioachwa na serikali iliyopita, kuongeza bajeti ya huduma za umma, kutoza kodi zaidi kwa matajiri na kuondoa mageuzi ya pensheni yanayolazimisha raia kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi kabla ya kustahiki mafao.

Maandamano hayo yametokea wakati Rais Emmanuel Macron na Waziri Mkuu mpya, Sebastien Lecornu, wakikabiliwa na shinikizo la kisiasa pamoja na changamoto ya kurekebisha hali ya kifedha ya taifa hilo lenye uchumi wa pili kwa ukubwa barani Ulaya.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Bruno Retailleau, amesema polisi wameondoa baadhi ya vizuizi vilivyowekwa na waandamanaji, vikiwemo vilivyokuwa mbele ya vituo vya mabasi jijini Paris. SOMA: Ufaransa yaitambua Palestina

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button