Uwekezaji zaidi watakiwa hifadhi Kilimanjaro

MOSHI: NAIBU Kamishina wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini, Stelia Ndaga amesema kuwa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) inahitaji wawekezaji zaidi kuwekeza ‘lodge na camp site’ ili kukidhi mahitaji ya watalii.

Ndaga amesema hayo baada wanachama na waajiri wa Chama Cha Wafanyakazi Serikali na Afya (TUGHE) zaidi ya 800 kutembelea Hifadhi ya Kilimanjaro na kufanikiwa kupanda Mlima Kilimanjaro na kuona baadhi ya vivutio katika hifadhu hiyo.

Amesema lodge na camp site zilizopo katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro bado hazikidhi mahitaji ya watalii kulala hivyo aliwapa nafasi TUGHE kuhamashisha wawekezaji wa ndani na nje kuweka katika nyumba za kulala katika hifadhi hiyo ili watalii waweza kulala karibu na mlima huo kabla na baada ya kupanda mlima huo mrefu Afrika na duniani kwa kusimama.

Aidha, Ndaga amesema kuwa hifadhi za kanda ya kaskazini ,ambazo ni pamoja na Kinapa,Anapa,Hifadhi ya Ziwa Manyara na Hifadhi ya Tarangire ni hifadhi zinazoingiza fedha nyingi za kigeni serikalini kuliko hifadhi zote 21 nchini kutokana na uwepo wa vivutio vizuri vinavyowavutio watalii wengi na kufanya watalii hao kuvutiwa na kuvitembelea.

Naibu Kamishina huyo amesema TUGHE wameunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya kitalii kwa kuwa watalii wa ndani wengi kutembelea vivutio vilivyoko katika Mlima Kilimanjaro ikiwemo maporomoko ya maji,mimea ya kipekee na mandhari yam lima Kilimanjaro maarufu kwa jina la ‘’Paa la Afrika’’.

‘’Watalii wa ndani zaidi ya 800 kufanya utalii wa ndani kwa wakati mmoja ni historia iliyoachwa katika hifadhi hiyo hivyo wengine wanapaswa kuiga TUGHE kwa juhudi hizo walizoamua kufanya,” amesema Ndaga.

Naye Katibu wa TUGHE Taifa, Henry Mkunda, alisema kuwa ziara hiyo imewapa uelewa mkubwa zaidi wa thamani na uzuri wa urithi wa dunia na wameunga mkono jitihada za Rais ambazo amekuwa akihimiza watalii wa ndani kutembelea vivutio vya ndani kwa lengo la kuvitangaza.

Mkunda amesema TUGHE imeweka historia kwa kupeleka watalii wa ndani zaidi ya 800 kwa wakati mmoja kutalii katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaaro na kusema kuwa hilo linapaswa kuungwa mkono na vyama vingine vya wafanyakazoi lengo likiwa moja kuunga mkono jitihada za Rais kutangaza vivutio vya utalii ili wageni waweze kumiminika nchini ili waweze kwenda katika hifadhi mbalimbali nchini.

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi TANAPA, Jully Bede Lyimo, aliongeza kuwa utalii wa ndani una faida nyingi zikiwemo kuongeza mapato, kuchochea ajira, kukuza biashara ndogo ndogo na kujenga uzalendo wa Taifa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro, Amri Mtekanga, aliwakaribisha wageni hao na kuwaeleza vivutio pamoja na taratibu za kupanda Mlima Kilimanjaro.

Ziara hiyo ya TUGHE imedhihirisha mshikamano wa Watanzania katika kuunga mkono sekta ya utalii kuelekea maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button