Samia aahidi neema kwa wachimbaji madini

RUVUMA : MGOMBEA wa kiti cha rais, kupitia Chama cha Mapinduzi, Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendelea kutoa kipaumbele uchimbaji salama kwa wachimbaji wadogo . Samia ameyasema hayo wakati wa mkutano wa kampeni ulifanyika katika uwanja wa VETA, Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
“Tutakwenda kuboresha wachimbaji wadogo lakini pia tutawaelekeza uchimbaji ambao utatunusuru kwenye vifo kwenye migodi ya uchimbaji.”
“Niseme pia kwamba mkoa huu umebarikiwa kuwa na madini mengi kuanzia dhahabu, shaba, makaa ya mawe, madini ujenzi na vito hadi urani yanapatikana ndani ya mkoa huu,” alisisitiza. Samia amesema kuwa endapo CCM ikipatiwa ridhaa, serikali yake itaanzisha na kuendeleza kongani za viwanda zinazohusiana na madini.
Amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza thamani ya madini kabla ya kuuzwa huku kipaumbele kikiwa katika uchimbaji na wachimbaji wadogo. SOMA: Waziri Mkuu kufungua maonesho ya madini Geita
Pia amesema wataendelea na mradi wa kuchimba madini ya urani na kuwa lengo la Serikali yake ni ya chakatwe na yasafishwe ndani ya nchi. “Nilifika wilayani Namtumbo kuzindua mradi wa madini ya urani pamoja na kuchimba madini hayo azma ya serikali yachakatwe, yasafirishwe kisha uwepo mtambo wa kuzalisha umeme nchini ili umeme wa uhakika upatikane, umeme ambao unakubalika duniani kama nishati safi.”