Dk. Nchimbi aahidi mambo saba Ludewa

LUDEWA : MGOMBEA mwenza kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk Emmanuel Nchimbi amesema wananchi wakiwachagua, serikali ya chama hicho itafanya mambo makubwa saba wilayani Ludema mkoani Njombe.
Dk Nchimbi alisema hayo katika mkutano wa kampeni katika Viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe jana. Alisema serikali itaimarisha mfumo wa ruzuku ya mbolea na mbegu ili kuongeza tija katika kilimo. Dk Nchimbi alisema serikali itajenga maghala sita mapya ya kuhifadhia nafaka na kutoa mashine tano za kubangua korosho pamoja na mashine nyingine tano mpya za kuchakata kahawa.
Alisema serikali itapanua mradi wa umwagiliaji katika mabonde matatu makuu ya wilaya hiyo ili kuongeza uzalishaji na ajira. Katika sekta ya uvuvi, Dk Nchimbi alisema vizimba vipya 50 vya kufugia samaki vitajengwa Ziwa Nyasa sambamba na kuongeza boti za doria ili kulinda rasilimali za uvuvi.
Pia, alisema serikali imedhamiria kujenga majosho mapya matano na machinjio ya kisasa mawili na kuongeza idadi ya wataalamu wa mifugo ili kuhakikisha wafugaji wanapata huduma bora. Dk Nchimbi alisema serikali ya CCM imedhamiria kuiboresha zaidi Hospitali ya Wilaya ya Ludewa kwa kuongezamajengo na wataalamu wa afya, ili wananchi wasilazimike kusafiri kutafuta huduma za msingi nje ya wilaya.
Aliahidi ujenzi wa vituo vipya vya afya 14, zahanati nne, shule za msingi mpya tano na kuongeza madarasa 340 pamoja na maabara 12 kwa ajili ya kuimarisha elimu ya sayansi. Kwa kuzingatia mahitaji ya mtoto wa kike, alisema serikali ya CCM itajenga mabweni mapya 14 katika shule za sekondari za wilaya hiyo. SOMA: Dk Biteko aagiza miundombinu vituo vya afya itunzwe
Katika eneo la maji, alisema zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wa mjini na asilimia 80 wa vijijini wanapata maji safi na salama na dhamira ya serikali kwa miaka mitano ijayo ni kuongeza upatikanaji hadi kufikia asilimia 90 vijijini na asilimia 95 mjini, kupitia kukamilisha miradi inayoendelea na kuanzisha miradi mipya katika kata zote 17.
Pia, alisema umeme ambao umesambazwa vijijini utasambazwa zaidi kufikia vitongoji 125 ambavyo havijapata huduma hiyo. Dk Nchimbi alisema zaidi ya barabara tisa zilizobainishwa katika Ilani ya CCM 2025/2030 zitajengwa kwa viwango mbalimbali sanjari na miradi mingine mikubwa ya maendeleo.
JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com