ADC yaahidi magari ya visima kila halmashauri

MOROGORO  : MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC), Wilson Mulumbe amesema serikali yake itahakikisha kila halmashauri nchini inapewa magari ya kuchimba visima vya maji.

Mulumbe alitoa ahadi hiyo wakati wa mkutano wa kampeni katika Mtaa wa Bomba la Zambia, Kata ya Kingolwira, Manispaa ya Morogoro.

Katika mkutano huo Mulumbe  alikuwa na mgombea mwenza wake, Shoka Khamis Juma. Mulumbe alisema tatizo la maji limeendelea kuwa kero kwa wananchi. Hivyo, wakimchagua serikali yake italipa kipaumbele suala hilo ili kuwaondolea adha wananchi.

Alisema ADC ina dira na mikakati ya kuleta maendeleo kupitia usimamizi bora wa rasilimali, uwazi katika utawala na kuondoa mianya ya ubadhirifu wa mali za umma.

Mulumbe alisema katika serikali ya ADC, wenyeviti wa serikali za mitaa watawekwa kwenye mfumo wa malipo kwa kupewa mishahara ili kutambua mchango wao katika kusimamia maendeleo ya wananchi.SOMA: ADC kufuta malipo kumuona daktari

Alisema serikali ya chama hicho itaboresha huduma za kijamii zikiwemo za elimu, afya, nishati na miundombinu ya barabara kwa lengo la kuimarisha ustawi wa Watanzania wote. Mulumbe alisema ilani ya uchaguzi ya ADC 2025-2030 imeweka mkakati kwa kutaka kila mwananchi apate huduma bora za elimu na afya bure, mikopo bila riba na haki sawa katika sekta zote za maisha.

Alisema ADC imeahidi kutoa elimu bure kuanzia mtoto anapo[1] zaliwa hadi kumaliza masomo na huduma za afya bure maisha yake yote. Pia, ilani ya chama hicho imepiga marufuku vizuizi vya kutoa huduma kwa maiti, ili familia zipate heshima na faraja bila gharama zisizo za lazima.

Chama hicho kupitia ilani yake kimependekeza mfumo wa elimu mbadala na mwanafunzi ataka[1] pomaliza darasa la saba ataelekez[1] wa kwenye mafunzo ya ufundi stadi ili kumpa ujuzi wa moja kwa moja wa kujipatia kipato.

ADC imependekeza mageuzi ya umri wa kustaafu na kwamba mtu atastaafu akifikisha miaka 70. Chama hicho kimeeleza serikali yake itaangalia kwa umakini kada muhimu ambazo zina wataalamu wachache au zinazohitaji ujuzi maalum kama vile madaktari bingwa, watafiti na wahandisi wa kiwango cha juu ili kuendeleza ajira zao kwa muda mrefu zaidi kadri inavyohitajika kwa maslahi ya taifa.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button