Danon: Hamas lazima iondolewe Gaza

ISRAEL : MWAKILISHI wa kudumu wa Israel katika Umoja wa Mataifa, Danny Danon, amesema kuwa suluhu ya mataifa mawili si jambo linalowezekana kwa Israel.
Kauli hiyo aliitoa kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa kimataifa wa usuluhishi wa amani kuhusu Palestina, unaosimamiwa na Ufaransa na Saudi Arabia kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Danon alisema Israel itaendelea na mapambano dhidi ya Hamas hadi pale itakapohakikisha kuwa kundi hilo halina ushawishi tena Gaza na mateka wote wamerejeshwa. SOMA: Nchi za Kiarabu,Kiislamu kujitenga na Israel
Aliongeza kuwa ni katika mazingira hayo pekee ambapo Israel inaweza kuzungumzia mustakabali wa baadae wa eneo hilo. Matamshi ya mwanadiplomasia huyo yanakuja wakati mataifa kadhaa, ikiwemo Ufaransa, yakiendelea kutangaza kulitambua rasmi taifa la Palestina, hatua inayoongeza shinikizo la kimataifa dhidi ya Israel.



