NEMC yashiriki kongamano la binadamu na hifadhi hai

CHINA: Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeshiriki Kongamano la Dunia la Programu ya UNESCO ya Binadamu na Hifadhi Hai lililofanyika Jijini Hangzhou nchini China kuanzia tarehe 22-25 Septemba 2025.
Kwa upande wa NEMC, kongamano hilo limehudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Baraza Dk. Immaculate Sware Semesi pamoja na Meneja wa Tafiti za Mazingira, Dk Rose Sallema.
Wawakilishi wengine kutoka Tanzania katika kongamano hilo ni kutoka TANAPA. Kongamano hilo limelenga kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, kupata maarifa na teknolojia mpya katika kusimamia na kuhifadhi mazingira nchini.
SOMA ZAIDI
Pia ni fursa katika uendelevu wa Hifadhi za Taifa, fursa za kutangaza vivutio vya kitalii, kuimarisha ushirikiano na Jamii , kuitangaza Tanzania kimataifa, kuvutia wawekezaji na kusaidia kufikia malengo ya maendeleo nchini.