Rihanna apata mtoto wa kike

MWANAMUZIKI nyota wa muziki wa Pop duniani, Rihanna, amejaaliwa mtoto wake wa tatu, binti, na mpenzi wake A$AP Rocky, nchini Marekani. Mtoto huyo amepewa jina la kisanii la babake na ujio wake umetangazwa kupitia ukurasa wa Instagram wa Rihanna, uliokuwa na picha za kifamilia pamoja na glovu ndogo za ndondi za rangi ya waridi.

Kwa wawili hao, hii ni familia ya tatu baada ya watoto wawili wa kiume, Riot na RZA. Rihanna alitangaza ujauzito wa hivi karibuni wakati wa hafla ya Met Gala mwaka huu. Habari za kuzaliwa kwa mtoto huyo zimepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki duniani kote, ambapo chapisho la Rihanna mtandaoni limevutia zaidi ya likes milioni tano ndani ya saa mbili. SOMA: Rihanna kuja na albamu ya tisa

Mbali na muziki, Rihanna mwenye umri wa miaka 37 amejipatia mafanikio makubwa kwenye biashara kupitia chapa yake ya urembo, Fenty Beauty, na kampuni ya mavazi ya ndani. Jarida la Forbes linakadiria thamani yake kuwa zaidi ya dola bilioni moja, jambo linalomfanya kubaki katika orodha ya wanawake maarufu na wenye ushawishi mkubwa duniani.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 6000-12000 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..

    HERE——————————————⊃⫸ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→ http://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button